Kwa mawasiliano zaidi.

Name

Email *

Message *

Wednesday, January 8, 2025

Shikira la Strong Women Foundation latoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto.

 Shirika la Strong Women Foundation (SWF) Tanzania lenye makao yake makuu jijini Mwanza.Limetoa vifaa vya shule kwa watoto wanaopitia mazingira magumu kituo cha Foundation Karibu Tanzania kilichopo jijini Mwanza.

Akiongea na mwandishi wetu Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo ambaye pia ni Muimbaji wa nyimbo za Injili Neema Ng'asha anasema namshukuru Mungu kuwawezesha kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto hawa. Pia anaomba jamii kuwakumbuka hawa watoto wengine ni yatima kabisa hawana wazazi.Qazazi wao ni Sisi tulio hai. Kutoa ni moyo hata kwa kidogo ulicho nacho ukiwakumbuka watoto hawa ni faraja kwao pia kwa Mungu unakuwa umewekeza.

Aidha Mkurugenzi wa Strong Women Foundation Neema Ng'asha amewashukuru sana wadau wote ambao wamekuwa wakimshika mkono kufanya kazi hii.

Strong Women Foundation (SWF)wakiwa kituo cha Foundation Karibu Tanzania.





Tuesday, January 7, 2025

Neema Ng'asha apata tuzo ya muimbaji bora wa kike kanda ya Ziwa

Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza Neema Ng'asha ameibuka kuwa mshindi wa Tuzo za Muimbaji bora wa nyimbo za injili kanda ya ziwa.Tuzo hizi ziliandaliwa na kampuni ya Eagle Entertainment iliyopo Sengerema ambapo mgeni rasmi wa usiku wa tuzo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda.

Akiongea na waandishi wa habari Neema Ng'asha anasema namshukuru sana Mungu kwa hatua hii aliyoifikia,ameanza kuimba rasmi mwaka 2010 amefanikiwa kuwa nominated kwenye tuzo kutoka Kenya na East Africa lakini hakubahatika kupata tuzo.Anamshukuru Mungu kwa hatua hii aliyofikia kwakua imeleta chachu nzuri kwenye huduma yake ya uimbaji.

Neema Ng'asha akiwa ameshilikia tuzo yake.





 

Tuesday, May 30, 2023

Strong Women Foundation(SWF) yaongea na watoto wa kike kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Mapema leo Strong Women Foundation (SWF) walitembelea shule ya msingi Mkolani,iliyopo jijini Mwanza  kuongea na watoto wa kike.

Strong Women Foundation ni shirika ambalo limejikita kuelimisha wanawake na watoto wa kike kutimiza ndoto zao.Leo lilifika shule ya Msingi Mkolani na kufanikiwa kuongea na watoto wakike waaweze kuepuka vishawishi na mimba za utoto ili waweze kutimiza ndoto zao.


Pia Mkurugenzi wa Shirika la Strong Women Foundation amewaasa kutokujihusisha na vitendo vya usagaji na ushoga na kukataa kipindi wanaona vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Taifa letu. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Strong Women Foundation,Neema  Ng'asha ameiomba pia jamii kuzingatia malezi bora ya watoto.Kuhakikisha wanafata elimu bora kwa kusimamia na pia kuwalinda na vitendo vya ushoga,ulawiti na ubakaji.


Meya wa jiji la Mwanza awa mgeni rasmi katika uzinduzi wa shirika la Strong Women Foundation (SWF)

 Meya wa jiji la Mwanza,Mheshimiwa Sima Costantine Sima,amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Shirika la Strong Women Foundation (SWF)lililopo jijini Mwanza.

            ( Mhe.Sima Costantine Sima akiongea)

Uzinduzi huu uliofanyika katika kumbuka wa Mwanza Hotel na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo jijini Mwanza 

  

(Mkurugenzi Mtendaji wa Strong Women Foundation Neema Ng'asha akiongea)

Shirika la Strong Women Foundation ni asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake makuu jijini Mwanza.Shirika hili linafanya kazi ya kusaidia wanawake,mabinti na watoto wanaopitia mazingira magumu.

(Bodi member wa Strong Women FoundationBeth Mpuya Gambaloya )

Katika uzinduzi huu Meya wa jiji la Mwanza Amepongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Strong Women Foundation Neema Ng'asha pamoja na viongozi wote wa shirika hilo kwa kazi njema wanayofanya kusaidia jamii yetu.

Bishop Daniel Moses Kulola pamoja na mke wake Mercy Daniel Kulola na wachungaji wengine wakifatilia kwa umakini uzinduzi huu



Kikundi cha MWANAMKE  NGUZO kutoka Strong Women Foundation wakimuuzia mgeni rasmi bidhaa walizotengeneza.


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Strong Women Foundation atoa mtaji kwa mama anayepitia mazingira magumu

 Mapema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Strong Women Foundation Neema  Ng'asha,amefanikiwa kumpa Mtaji wa biashara ndogo mama anayepitia mazingira magumu,jijini Mwanza.

Neema Ng'asha ameiomba jamii kuwawezesha wanawake wenye moyo wa kufanya biashara ndogo ndogo kwa kuwapa mitaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Pia ameomba wanawake kufanya kazi kwa bidii na kuomba msaada kwa wadau wawawezeshe pale wanapokwama kutimiza malengo yao.

Ni muhimu pia wanawake kujiunga katika vikundi na kujifunza kazi mbalimbali za ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi na wasiwasi tegemezi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Strong Women Foundation apeleka msaada wa chakula kwa watoto wanaoishi mazingira magumu

Mkurugenzi mtendaji  wa Strong Women Foundation,lililopo jijini Mwanza Neema Ng'asha,leo amekwenda kuwapa msaada wa chakula watoto wanaopitia mazingira magumu.Ameiomba jamii kuwa kumbuka watoto wanaopitia mazingira magumu kwa kuwapata chakula na kuhakikisha wanapata elimu na malezi bora.



Pia ameomba wadau wenye moyo wa kusaidia jamii waungane na taasisi zinazofanya kazi ya kusaidia jamii kwa ujumla tuweze kuleta mabadiliko makubwa kwa jamii yetu.

Kama kuna mtu ataguswa kuwa mmoja wa wadau wa Strong Women Foundatio tunaomba awasiliane nasi kwa namba 0754 220078.





 

Monday, September 5, 2022

WAJUMBE WA BODI PAMOJA NA BAADHI YA WAFANYAKAZI WA STRONG WOMEN FOUNDATION.

 

Wajumbe wa bodi pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Strong Women Foundation wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Team hii inafanya kazi kubwa sana kuhakikisha inatimiza malengo yake kusaidia wanawake na mabinti Tanzania.

Kushoto ni Mr Michael Petro Kaaya (Gender& Children Affairs Officer),Neema Ng'asha (Mkurugenzi mtendaji wa Strong Women Foundation),Christina Msegu(Research &Planning Officer),Beth Mpuya Gambaloya(Mhazini mkuu  na founder member) na Neema Petro Eliya(Founder  member wa Strong Women Foundation ).

Shikira la Strong Women Foundation latoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto.

 Shirika la Strong Women Foundation (SWF) Tanzania lenye makao yake makuu jijini Mwanza.Limetoa vifaa vya shule kwa watoto wanaopitia mazing...