Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza Neema Ng'asha ameibuka kuwa mshindi wa Tuzo za Muimbaji bora wa nyimbo za injili kanda ya ziwa.Tuzo hizi ziliandaliwa na kampuni ya Eagle Entertainment iliyopo Sengerema ambapo mgeni rasmi wa usiku wa tuzo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda.
Akiongea na waandishi wa habari Neema Ng'asha anasema namshukuru sana Mungu kwa hatua hii aliyoifikia,ameanza kuimba rasmi mwaka 2010 amefanikiwa kuwa nominated kwenye tuzo kutoka Kenya na East Africa lakini hakubahatika kupata tuzo.Anamshukuru Mungu kwa hatua hii aliyofikia kwakua imeleta chachu nzuri kwenye huduma yake ya uimbaji.

No comments:
Post a Comment