Strong Women Foundation ni shirika ambalo limejikita kuelimisha wanawake na watoto wa kike kutimiza ndoto zao.Leo lilifika shule ya Msingi Mkolani na kufanikiwa kuongea na watoto wakike waaweze kuepuka vishawishi na mimba za utoto ili waweze kutimiza ndoto zao.
Pia Mkurugenzi wa Shirika la Strong Women Foundation amewaasa kutokujihusisha na vitendo vya usagaji na ushoga na kukataa kipindi wanaona vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Taifa letu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Strong Women Foundation,Neema Ng'asha ameiomba pia jamii kuzingatia malezi bora ya watoto.Kuhakikisha wanafata elimu bora kwa kusimamia na pia kuwalinda na vitendo vya ushoga,ulawiti na ubakaji.



No comments:
Post a Comment