Strong Women Foundation imelenga zaidi kusaidia wanawake/mabinti wanaoishi katika mazingira magumu katika jamii yetu pia inasaidia watoto na vijana.
Malengo yetu ni kuona tunabadili maisha ya wanawake wa Tanzania kifikra na kiuchumi.
Tunaandaa semina za wanawake na mabinti ambazo zitawajengea uwezo wa kujiamini kuwa inawezekana haijalishi mazingira wanayopitia.Pia semina za ujasiriamali tunazoandaa zitasaidia wanawake na mabinti kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara ndogo ndogo.
Pichani ni baadhi ya wanawake waliohudhiria semina zetu.

No comments:
Post a Comment