Kwa mawasiliano zaidi.

Name

Email *

Message *

Wednesday, January 8, 2025

Shikira la Strong Women Foundation latoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto.

 Shirika la Strong Women Foundation (SWF) Tanzania lenye makao yake makuu jijini Mwanza.Limetoa vifaa vya shule kwa watoto wanaopitia mazingira magumu kituo cha Foundation Karibu Tanzania kilichopo jijini Mwanza.

Akiongea na mwandishi wetu Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo ambaye pia ni Muimbaji wa nyimbo za Injili Neema Ng'asha anasema namshukuru Mungu kuwawezesha kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto hawa. Pia anaomba jamii kuwakumbuka hawa watoto wengine ni yatima kabisa hawana wazazi.Qazazi wao ni Sisi tulio hai. Kutoa ni moyo hata kwa kidogo ulicho nacho ukiwakumbuka watoto hawa ni faraja kwao pia kwa Mungu unakuwa umewekeza.

Aidha Mkurugenzi wa Strong Women Foundation Neema Ng'asha amewashukuru sana wadau wote ambao wamekuwa wakimshika mkono kufanya kazi hii.

Strong Women Foundation (SWF)wakiwa kituo cha Foundation Karibu Tanzania.





Tuesday, January 7, 2025

Neema Ng'asha apata tuzo ya muimbaji bora wa kike kanda ya Ziwa

Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza Neema Ng'asha ameibuka kuwa mshindi wa Tuzo za Muimbaji bora wa nyimbo za injili kanda ya ziwa.Tuzo hizi ziliandaliwa na kampuni ya Eagle Entertainment iliyopo Sengerema ambapo mgeni rasmi wa usiku wa tuzo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda.

Akiongea na waandishi wa habari Neema Ng'asha anasema namshukuru sana Mungu kwa hatua hii aliyoifikia,ameanza kuimba rasmi mwaka 2010 amefanikiwa kuwa nominated kwenye tuzo kutoka Kenya na East Africa lakini hakubahatika kupata tuzo.Anamshukuru Mungu kwa hatua hii aliyofikia kwakua imeleta chachu nzuri kwenye huduma yake ya uimbaji.

Neema Ng'asha akiwa ameshilikia tuzo yake.





 

Shikira la Strong Women Foundation latoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto.

 Shirika la Strong Women Foundation (SWF) Tanzania lenye makao yake makuu jijini Mwanza.Limetoa vifaa vya shule kwa watoto wanaopitia mazing...